Mkutano wa 18 wa kimataifa kuhusu ugonjwa wa ukimwi ulifungwa tarehe 23 mjini Vienna, Austria. Ujumbe mkuu uliotolewa na mkutano huo wa siku 6 ni kwamba mwelekeo wa jumla wa hali mbaya ya maambukizi ya ukimwi duniani umekuwa ukidhibitiwa, lakini kuushinda ugonjwa huo bado kunahitaji juhudi kubwa.
Washiriki wa mkutano huo wametoa mwito kwa kauli moja wakitaka fedha nyingi zaidi zitengwe kwa ajili ya kukinga na kudhibiti ugonjwa wa ukimwi. Mwito huo umetolewa kutokana na wasiwasi wa nchi zinazoendelea kwamba wakati msukosuko wa fedha unapoendelea duniani, nchi zilizoendelea zitapunguza fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukinga na kudhibiti ugonjwa wa ukiwmi, hususan kupunguza msaada kwa nchi zinazoendelea.
Washiriki wa mkutano huo pia wanaona kuwa njia kuu za kuambukiza ukimwi duniani kwa sasa ni kutumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano, na ngono isiyo salama, na hali ya maambukizi ya ugonjwa huo miongoni mwa vijana ni mbaya sana, kwa hiyo nchi mbalimbali duniani zinatakiwa kutilia maanani kazi ya kukinga ugonjwa huo, hasa kuwaelimisha vijana kuhusu ugonjwa huo, ili kuwaongezea mwamko wa kujilinda na kuwalinda wengine.
0 comments:
Post a Comment