
Huyo hapo juu ndie Katibu Mstaafu wa TSAH,Bw ABDALLAH MBAROUK akiwa tayari kwa safari yake ya kuelekea Nyumbani Tanzania baada ya kumalizika kwa mda wake wa masomo hapa India.

Hapo kama mnavyomuona Bw.Abdallah mbarouk akipata kumbukumbu na Mwenyekiti wetu kwa sasa Bw.Abdillah Nkya.

Katibu mstaafu akiwa pamoja na mdau mkuu wa urary95 Bw.Mustafa Said a.k.a Tata boy kama mnavyomuona akasema katibu uwezi kuniacha bure lazima tupate kumbukumbu ya pamoja nami.

Ulifika mda wa kupata kumbukumbu ya pamoja na Katibu Mstaafu kabla ya kuanza kwa safari yake,Kutoka kushoto ni .Ankali Nass,Toto janja Blest,Bw,Samwel,Bw.Saddallah Mbeyu(Makamu Mwenyekiti Mstaafu)nyuma yake ni Mimi,anaefuata Bw.Ahmed,Bw.Abdallah na mwisho kabisa ni Mwenyekiti wetu Bw.Abdillah Nkya

kama kawaida desturi yetu kupata kumbukumbu kama hizi ankali Nass akiaga kwa niaba ya wadau wote

Hapa naona msafiri kama anawasiliana na ndugu na jamaa huku akifurahi anawaambia kuwa yupo njiani anakwenda nyumbani wakae tayari kwa kumpokeaaa.

Bw.Samweli alimuomba msafiri kupata kumbukumbu ya pamoja naye huku anakli Nass nae akiwasili eneo la tukio kwa tabasamu kali sana

Baada ya Msafiri kuingia ndani tayari kwa safari huku nje hatukua bure kwani nasi tulihitaji kumbukumbu za hapa na pale kama unavyojua uwanja wa kimataifa wa Shamshabad hapa Hyderabad unavyovutia usiku unaweza kusema mchana,Kutoka kushoto Ankali Nass,nyuma yake Ahmed,anaefuata Mimi,Makamu Mstaafu Bw.Saddallah Mbeyu,mwisho kabisa Toto janja Blest

Ankali Nass akifurahia jambo hapa

Mimi nikiwa na Mwenyekiti wangu hapa Bw.Abdillah Nkya

Makamu Mwenyekiti mstaafu naye akuwa nyuma katika swala zima la kupata kumbukumbu ndani ya Shamshabad Airpot

Bw.Ahmed Mwinyially mmoja kati ya wadau wangu akipata kumbukumbu naye pia

Mdau Ahmed aliniomba tupate kumbukumbu japo moja tukiwa uwanjani hapo huku tukiwa tayari kabisa kwa kurejea nyumbani kwani msafiri tayari alikuwa kashamaliza taratibu zote ndani.
0 comments:
Post a Comment