MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic
ameingia kutetea tuzo yake ya Bao Bora la Mwaka, baada ya kutajwa katika orodha
ya wanaowania tuzo ya Puskas 2014.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
33 ni miongoni mwa wachezaji 10 walioingia kwenye orodha fupi iliyoandaliwa na
FIFA, fbaada ya bao lake alilofunga dhidi ya Bastia katika Ligue 1 akiichezea
klabu yake, Paris Saint-Germain ya Ufaransa.
Msweden huyo alishinda tuzo hiyo
msimu uliopita kwa bao la umbali wa mita 30 alilofunga dhidi ya England katika
ushindi wa 4-2 kwenye mchezo wa kirafiki.

Mshindi wa Puskas 2013, Zlatan
Ibrahimovic ameingia tena kuwania tuzo hiyo
Ibrahimovic anachuana na wakali kama
Diego Costa na Robin van Persie kwenye orodha hiyo ya wachezaji 10 ya FIFA
ambayo inatokana na maelfu ya mabao yaliyofungwa kati ya Oktoba 3, mwaka 2013
hadi Septemba 26.
Mashabiki
watapiga kura hadi Desemba 1 kwenye Tovuti ya FIFA ambako orodha ya wachezaji 10 itaopungua
hadi kubaki watatu.
Tuzo hizo zilizoanzishwa mwaka 2009,
zikipewa heshima ya gwiji wa zamani wa Hungary na Real Madrid, Ferenc Puskas,
imekwishachukuliwa na nyota kama Cristiano Ronaldo, Hamit Altintop, Neymar,
Miroslav Stoch pamoja na Ibrahimovic miaka iliyopita.
Ibrahimovic alishinda
tuzo hiyo mwaka jana baada ya bao aliloifungia Sweden kwa tik tak katika
ushindi wa 4-2 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya England
0 comments:
Post a Comment