Searching...
Thursday, October 9, 2014

WAKALA ALIYEWAPELEKA FALCAO NA DI MARIA MAN UNITED AZUNGUMZIA SAFARI YA RONALDO OLD TRAFFORD akiri Mreno huyo ana mapenzi na United lakini...

Ronaldo has already scored 13 goals in six appearances for Real Madrid this season
WAKALA wa Cristiano Ronaldo - Jorge Mendes ametupilia mbali uwezekano wa mshambuliaji huyo kurejea Manchester United na kusema supastaa huyo wa Kireno atamalizia soka lake Real Madrid wakati atakapotimiza umri wa miaka 40.
Jorge Mendes akaenda mbali zaidi kwa kusema hata tokea mchezaji mzuri kama Ronaldo kwa miaka 500 ijayo.
Hata hivyo wakala huyo ambaye alihusika katika safari ya Radamel Falcao na Angel di Maria kwenda Manchester United, amekiri kuwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 bado ana mapenzi na Manchester United.
Ronaldo spent six years at Old Trafford and still has a soft spot for Manchester United
Lakini akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha TV cha Hispania,  Jorge Mendes alisema hakuna kabisa uwezekano wa Ronaldo kuondoka Real Madrid.
Mendes akasema: “Ronaldo atamaliza soka lake Real Madrid akitimiza umri wa miaka 40. Ronaldo mchezaji bora kuwahi kutokea. Anaimarika siku hadi siku.
“Kamwe hatatokea mchezaji kama yeye kwa miaka 500 ijayo.”

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!