MSHAMBULIAJI
Robin van Persie amepuuzia madai kwamba matatizo yake ya goti ndiyo
yameifanya Manchester United imsajili Radamel Falcao, na amesema
anajiandaa kufanya kazi na mkali huyo mpya.
Iliripotiwa
kwamba kocha Louis van Gaal alikuwa anahofia majeruhi ya Mholanzi
mwenzake huyo kama angehitaji upasuaji na ndiyo maana akatoa Pauni
Milioni 6
kumsajili Falcao kwa mkopo, lakini Van Persie amesema maneno hayo
hayana maana hata kidogo na atapambana kupata nafasi ya kucheza na
Mcolombia huyo.
Washirika watatu: Van Gaal atalazimika kuumiza kichwa katika kuipanga safu yake ya ushambuliaji msimu huu
"Inanifurahisha
watu wanavyotengeneza maneno ya uzushi namna hii. Sijui yanatoka wapi
na naweza kusema na mono wangu ukiwa moyoni mwangu kwamba sitakwenda
kufanyiwa upasuaji hospitali.
Falcao atavaa jezi namba 9 Old Trafford baada ya kusajiliwa kwa mkopo kutoka Monaco na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atakuwa analipwa kiasi cha Pauni 280,000 kwa wiki.
Na katokana
na rekodi yake nzuri ya kufunga mabao ukilinganisha na kwamba Wayne
Rooney ameteuliwa kuwa Nahodha wa timu, inafikiriwa Van Persie atasotea
namba kikosi cha kwanza. Lakini mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal amesema anakaribisha ushindani wa namba.
"Nakaribisha
ujio wake, atatufanya tube bora. Katika klabu kubwa lazima wakati wote
uwe na wachezaji bora, ambayo pia ndiyo falsafa yangu. Falcao lazima apiganie nafasi yake, nami pia kadhalika. Lazima tupambane na Wayne Rooney na James Wilson kuona nani watacheza.
Van
Persie ameukosa mwanzo wa msimu baada ya kupewa mapumziko kufuatia
kumalizika kwa Kombe la Dunia, lakini alicheza kwa dakika 60 dhidi ya
Burnley mwishoni mwa wiki.
0 comments:
Post a Comment