MABAO mawili ya Thomas Muller yameipa Ujerumani ushindi wa 2-1 dhidi ya Scotland katika mchezo wa kufuzu fainali za Euro 2016.
Mshambuliaji
huyo wa Bayern Munich aling'ara mno katika mchezo huo na kuendeleza
mafanikio ya Ujerumani baada ya kutwaa Kombe la Dunia akifunga dakika za
18 na 70, wakati bao la Scotland limefungwa na Ikechi Anya dakika ya
66.
Nyota
huyo alifunga mabao yake ya 24 na 25 katika mechi 58 dhidi ya Scotland
iliyomaliza na wachezaji 10 baada ya Charlie Mulgrew kutolewa kwa kadi
nyekundu dakika za majeruhi.
0 comments:
Post a Comment