Searching...
Tuesday, September 2, 2014

FALCAO ALIVYOTAMBULISHWA MANCHESTER UNITED

KLABU ya Manchester United imemtambulisha rasmi mshambuliaji Radamel Falcao baada ya kukamilisha uhamisho wake katika siku ya mwisho ya kufungwa pazia la usajili.
Mpachika mabao huyo wa Monaco aria wa Colombia aliwasili kwa ndege binafsi kusaini mkataba wa mkopo wa muda mrefu wa msimu Old Trafford kwa ada ya Pauni Milioni 6, ambao unatoa fursa ya kununuliwa moja kwa moja kwa Pauni Milioni 46.
Falcao ameiambia www.manutd.com: "Nina furaha kujiunga na Manchester United kwa mkopo msimu huu. Manchester United ni klabu kubwa duniani na wazi inatakiwa kurudi juu,"amesema mchezaji huyo ambaye ameweka wazi hamu yake ya kufanya kazi na kocha Louis van Gaal ili kutoa mchango wake kuirudisha juu klabu hiyo.
Side by side: Falcao poses with the United shirt and assistant manager Ryan Giggs
Falcao akiwa ameshika kwa pamoja jezi ya United na kocha Msaidizi wa timu hiyo, Ryan GiggsSide by side: Falcao poses with the United shirt and assistant manager Ryan Giggs
Nyota huyo wa Colombia anakuwa mchezaji wa nane kutoka nchi hiyo kucheza Ligi Kuu ya England

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!