Searching...
Monday, August 18, 2014

MANUEL PELLEGRINI AONYA KIKOSI CHAKE NI BORA KULIKO MWAKA MMOJA ULIOPITA

Confident: Manuel Pellegrini is adamant that his title-winning City squad has progressed during his first year
Anajiamini: Manuel Pellegrini anaamini kikosi chake cha ubingwa kimeimarika zaidi kwa kipindi chake cha mwaka mmoja.

KOCHA wa Manchester City, Manuel Pellegrini anajiamini kuwa kikosi chake kilichoshinda ubingwa msimu uliopita kimekuwa bora zaidi msimu huu.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu England walizindua kampeni zao za EPL kwa kuitandika Newcastle United mabao 2-0 jana jumapili.
Pellegrini alifurahishwa na ushindi huo licha ya wachezaji wake wengi waliocheza kombe la dunia kutokuwa fiti ipasavyo.
Lakini anajua kuwa kutakuwa na ushindani mkubwa kwa mara nyingine tena msimu huu, ila ameonya kuwa kikosi chake kimeimarika zaidi chini yake.
Champions: Manuel Pellegrini won the Premier League title during his first year in English football last season
Mabingwa: Manuel Pellegrini alishinda taji la ligi kuu England msimu uliopita.

Alisema: "Ni ngumu sana kufananisha kila mwaka. Labda msimu uliopita watu wengi walinihofia kuwa sitaweza kutwaa ubingwa kwasababu ulikuwa msimu wangu wa kwanza wa ligi kuu England".
"Leo tuna mwaka mmoja tukifanya kazi na kikosi na nadhani pia tuna kikosi bora".
"Lakini siku zote England kuna timu tano au sita ambazo zinaweza kutwaa ubingwa, hivyo njaa tuliyoanza nayo katika mechi ya kwanza tunatakiwa kuendelea na wewe".

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!