Searching...
Thursday, August 28, 2014

Mabingwa Bundesliga Bayern Munich wametangaza kukubaliana na mabingwa Ulaya klabu ya Real Madrid juu ya uhamisho wa Kiungo mkongwe Xabi Alonso, kuziba nafasi za majeruhi zilizoachwa na Javi Martinez, Bastian Shwanstiger na Thiago Alcantara.

Bayern Munich have made a move for Xabi Alonso
Xabi Alonso


Akithibitisha mbele ya waandishi wa Habari, mkurugenzi wa bodi ya Bayern munich, Jan-Christian Jeseen,  amesema kuwa klabu hizo zimekubaliana kuhusu uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri wamika 32 na anafanyiwa vipimo vya afya leo Agosti 28, 2014. 

Alonso alijiungana Real Madrid mwaka 2009, akitokea Liverpool na kufanikiwa kuichezea Madrid mechi zaidi ya 200, mkataba wa awali wa Alonso ulikuwa unamalizika mwaka 2016, lakini analazimika kuondoka Santiago Bernabeu kutokana na ugumu wanafasi katika kikosi cha kwanza cha Carlo Anchellot kutokana na uwepo wa Toni Kroos aliye jiunga na klabu hiyo akitokea Bayern Munich Julai mwaka huu.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!