Searching...
Monday, August 4, 2014

DROGBA ARUDI NA MGUU MBAYA CHELSEA, ASHINDWA KUNG'ARA WAKIPIGWA 3-0 UJERUMANI

MKONGWE Didier Drogba ameshindwa kung'ara akiichezea Chelsea kwa mara ya kwanza tangu arejee msimu baada ya kuchapwa mabao 3-0 Werder Bremen nchini Ujerumani katika mchezo wa kujiandaa na msimu.
Mshambuliaji huyo wa Ivory Coast, aliichezea kwa mara ya mwisho Chelsea mwaka 2012 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikishinda kwa penalti dhidi ya Bayern Munich, lakini leo akirejea Ujerumani yeye na washambuliaji wengine wa The Blues- walilala kwa mabao ya Ludovic Obraniak kwa kichwa na penalti za Assani Lukimya na Felix Kroos.
Amerudi na mguu mbaya: Didier Drogba ameichezea tena kwa mara ya kwanza The Blues leo tangu arejee na imefungwa 3-0
Beaten: Chelsea goalkeeper Thibaut Courtois conceded two goals in Germany
Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois amefungwa mabao mawili leo, wakati bao lingine alifungwa Petr Cech kipindi cha pili

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!