MSHAMBULIAJI Lazar Markovic ataigharimu Liverpool Pauni Milioni 20 leo atakapothibitishwa kusajiliwa na kocha Brendan Rodgers.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Serbia aliwasili Merseyside Jumapili usiku kwa
ajili ya kukamilisha vipimo vya afya katika hospitali ya Spire Liverpool
iliyopo viwanja vya mazoezi vya klabu, Melwood baada ya Liverpool
kukubali kutoa Pauni Milioni 20 kumnunua kutoka Benfica.

Markovic akiwa ameshika jezi ya Liverpool Uwanja wa Anfield
Liverpool
imekuwa ikimfukuzia kwa muda mrefu Markovic hata kabla Luis Suarez
hajahamia Barcelona – na wanataka kufanya jithada za haraka kupata
mshambuliaji hatari kinda Ulaya.
Markovic,
ambaye alitoa mchango mkubwa kwa Benfica kutwaa taji la Ligi Kuu ya
Ureno msimu uliopita, amekubali mkataba wa muda mrefu na ataungana na
Rickie Lambert, Adam Lallana na Emre Can katika orodha ya wachezaji
wapya wa timu hiyo iliyoshika nafasi ya pili Ligi Kuu England Mei mwaka
huu nyuma ya Manchester City.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 20 hatokuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa
Liverpool, kwani timu hiyo bado inawataka mshambuliaji wa Ubelgiji,
Divock Origi na beki wa kushoto wa Sevilla, Alberto Moreno.




0 comments:
Post a Comment