Searching...
Wednesday, May 14, 2014

RADAMEL FALCAO ATAJWA KIKOSI CHA AWALI CHA COLOMBIA KOMBE LA DUNIA

385552_heroaKOCHA wa timu ya taifa ya Colombia, Jose Pekerman amemtaja Radamel Falcao  katika kikosi chake cha awali cha wachezaji 29 kwa ajili ya kombe la dunia nchini Brazil kuanzia mwezi ujao.
Nyota huyo wa klabu ya Monaco alikuwa katika hatihati ya kushiriki kombe la dunia kutokana na kuumia vibaya goti lake kwenye mchezo wa Coupe de France mwezi junuary mwaka huu.
Hata hivyo mwezi uliopita  nyota huyo wa zamani wa Atletico  Madrid alisema anahitaji mwezi mmoja kuimarika zaidi, lakini Pekerman ameamua kumujumuisha mshambuliaji huyo hatari.
Falcao alifunga mabao 9 katika mechi 13 za kuwania kufuzu kombe la dunia na alishirikiana vizuri sana na wachezaji,
 Jackson Martinez  na mchezaji wa Borussia Dortmund, Adrian Ramos.
Colombia wataanza kampeni zao za kombe la dunia katika kundi C dhidi ya Ugiriki Juni 14.
Kikosi kizima:
Walinda mango: Faryd Mondragon (Deportivo Cali), David Ospina (Nice), Camilo Vargas (Independiente Santa Fe)
Walinzi: Santiago Arias (PSV), Pablo Armero (Napoli), Eder Alvarez Balanta (River Plate), Aquivaldo Mosquera (America), Luis Perea (Cruz Azul), Carlos Valdes (San Lorenzo), Mario Yepes (Atalanta), Cristian Zapata (Milan), Camilo Zuniga (Napoli)
Viungo: Abel Aguilar (Toulouse), Juan Cuadrado (Fiorentina), Fredy Guarin (Inter), Victor Ibarbo (Cagliari), Alex Mejia (Atletico Nacional), Juan Fernando Quintero (Porto), Aldo Ramirez (Morelia), James Rodriguez (Monaco), Carlos Sanchez Moreno (Elche), Elkin Soto (Mainz), Macnelly Torres (Al Shabab), Edwin Valencia (Fluminense)
Washambuliaji: Carlos Bacca (Sevilla), Radamel Falcao (Monaco), Teofilo Gutierrez (River), Jackson Martinez (Porto), Luis Muriel (Udinese), Adrian Ramos (Hertha Berlin)

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!