Masaa
24 baada ya vyombo vya habari vya Uingereza kuripoti kwamba kiungo wa
Bayern Munich Toni Kroos yupo tayari kuhamia Manchester United kutoka
Munich katika kipindi cha usajili kijacho, leo hii wakala wa mchezaji
huyo amezungumza na kuweka wazi kuhusu taarifa hizo.
Bild,
gazeti la Ujerumani, limeripoti kwamba wakala wa Kroos, Volker Struth
ametoa taarifa ambayo itawavuja moyo washabiki wengi wa United. Struth
aliiambia Bild:
"Kwa
muda mrefu sasa tumekuwa tukisikia kuhusu hizi tetesi na tukaamua kukaa
kimya. Lakini mpaka sasa naamini Toni atabaki Allianz Arena mpaka
2015."
Kroos
ana mkataba na Bayern mpaka 2015, lakini mapaka sasa amegoma kuongeza
mkataba mpya na Bayern. Anaripotiwa kulipwa €86,000 kwa wiki, na amekuwa
akiripotiwa kutaka mara mbili ya fedha anayolipwa sasa ili aendelee
kubaki klabu hapo.
0 comments:
Post a Comment