Searching...
Wednesday, April 30, 2014

MRUNDI ANAYETAKIWA SIMBA, WAZUNGU WATIA MKONO


Wakati Simba imeshaanza harakati za kumnasa Amissi Cedric ili ajiunge nayo msimu ujao, kuna taarifa timu za Ubelgiji na Ulaya Mashariki zimeanza mipango ya kumnasa.

Cedric, raia wa Burundi, anayekipiga katika kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda, amekuwa kivutio kwa Simba tangu msimu uliopita na siku chache zilizopita ilifanya naye mazungumzo baada ya kuja nchi akiwa na timu yake ya taifa ya Burundi ambayo ilishinda kwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki jijini Dar.
Kocha Mkuu wa Kenya, Harambee Stars, Adel Amrouche, amelithibitishia Championi Jumatano kuwa, Cedric sasa ni lulu nchini Ubelgiji anakotokea.
“Ni kweli kuna zaidi ya timu mbili za daraja la pili na daraja la kwanza ambazo zinamtaka Amissi, hata jana nimezungumza naye,” alisema Amrouche ambaye aliwahi kumfundisha mshambuliaji huyo wakati akiwa Kocha Mkuu wa Burundi kabla ya kutua Harambee Stars.
“Lakini kuna timu moja kutoka Ulaya Mashariki pia imeonyesha nia ya kutaka kumchukua, sasa sijui kama Simba itawahi au vipi.”
Ukiachana na Amrouche, Kocha Mkuu wa Rayon Sports, Luc  Eymael raia wa Ubelgiji ameliambia gazeti hili, tayari mchezaji huyo ana mwaliko mmoja wa kufanya majaribio Ubelgiji anakotokea.
“Nafikiri anaweza kwenda Ubelgiji kufanya majaribio kwenye klabu ya daraja la pili, viongozi waliniambia kuhusiana na hilo lakini sina uhakika itakuwa ni lini. Ligi imebakiza mechi moja kwisha, hivyo anakuwa huru kwenda,” alisema.

Cedric ndiye mfungaji bora wa Rwanda msimu uliopita baada ya kutupia nyavuni mabao 16, lakini pia anaongoza msimu huu akiwa na mabao 13 huku akiwa na nafasi kubwa ya kuitwaa nafasi hiyo kwa mara nyingine.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!