Searching...
Tuesday, April 15, 2014

LUIS FIGO KUJA NA REAL MADRID KUKIPIGA JIJINI DAR


Kikosi cha wachezaji nyota na wakongwe wa Real Madrid ya Hispania kinatarajia kutua nchini wakati wowote kabla ya mwaka huu kwisha kucheza mechi ya kirafiki.

Kikosi hicho kitakuwa na nyota mbalimbali kama Luis Figo, Michel Salgado, Christian Karembeu na wengine wengi ambao watatangazwa baadaye.
RAYCO GARCIA AKIWA NA SALEH ALLY

RAYCO GARCIA (KULIA) AKIWA NA RONALDINHO WAKATI AKIKIPIGA TIMU YA VIJANA YA BARCELONA
Mchezaji wa zawani wa timu za vijana za Real Madrid na Barcelona, Rayco Garcia amemuambia SALEHJEMBE kuwa mechi hiyo itakuwa ndani ya mwaka huu kama kila kitu kitaenda vizuri.

“Nimefika hapa Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya maandalizi, kuangalia mazingira.
RAYCO GARCIA (KUSHOTO) AKIWA NA LIONEL MESSI

“Lakini kuna watu maalum ambao wanashughulikia mechi hii kufanyika hapa.
“Shirikisho la soka la hapa, pia wana taarifa na wanajua maaendeleo ya suala hili. Hivyo tunataka kuangalia mambo yataenda vipi,” alisema Garcia aliyekuwa ameongozana na beki wa zamani wa Simba, Talib Hilal ambaye pia ni kocha wa timu ya taifa ya ufukweni ya Oman.
Garcia ndiye alisimamia ziara ya timu mbili za Real Madrid na Barcelona za wakongwe ambazo zilicheza mechi ya kirafiki Muscat, Oman mwezi uliopita na Madrid kupoteza kwa mabao 2-1.

Alisema wakongwe wawili, Zinedine Zidane na Roberto Carlos ambao ni makocha wa Real Madrid na Besiktas ya Uturuki, hawatakuwa na nafasi ya kuja na timu hiyo nchini kama mpangilio wa ziara hiyo utawezekana.
RAYCO GARCIA AKIWA  CAMP NOU

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!