Searching...
Wednesday, April 23, 2014

GIGGS KATIKA SIKU YA KWANZA KAZINI MAN UNITED NA PAUL SCHOLES

MKONGWE Ryan Giggs alionekana vizuri na aliye tayari kwa kazi Manchester United wakati anawasili kazini leo katika siku ya kwanza tangu kutangazwa kuwa mrithi wa muda wa David Moyes. 
Giggs amepewa ukocha wa muda wakati mchakato wa kumsaka kocha mpya unaendelea, kufuatia kuondoka kwa Moyes baada ya miezi 10 tu ya Mkataba wake wa miaka sita.  
Gwiji huyo wa Wales aliwasili katika Uwanja wa mazoezi wa klabu, Carrington Saa 2.10 leo asubuhi kabla ya Wayne Rooney, Rio Ferdinand, Michael Carrick na nyota wengine wa United kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Norwich mwishoni mwa wiki.  
Kazini mapema: Ryan Giggs akiendesha kuelekea Uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington leo asubuhi

Wakati huo huo: Mkongwe mwingine wa timu hiyo, Paul Scholes alihudhuria programu kamili ya mazoezi leo Carrington baada ya kurejeshwa klabuni kama mmoja wa maofisa wa benchi la Ufundi.
Ilielezwa jana kwamba mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 39 atafanya kazi chini ya Ryan Giggs, aliyerithi mikoba ya David Moyes.
He's back: Paul Scholes, pictured training with Wayne Rooney during his playing days, has returned to Manchester United as part of the coaching team following the sacking of David Moyes
Amerudi: Paul Scholes akiwa na Wayne Rooney mazoezini enzi zake anacheza, leo amefika kama kocha baada ya kufukuzwa kwa David Moyes

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!