Rekodi
za ufungaji wa mabao wa washambuliaji wa Liverpool Luis Suarez na
Daniel Sturridge msimu huu ni bora kuliko zote katika ligi kuu ya EPL
tangu msimu wa 1965.
Suarez
na Sturridge sio tu kwamba wanaongoza kwa ufungaji wa mabao na kushika
nafasi mbili za juu katika msimamo wa ufungaji katika EPL, lakini hawa
ndio washambuliaji pea ambao wamefunga mabao angalau mabao 18 kila mmoja
katika hatua hii ya msimu tangu walipofanya hivyo washambuliaji wawili
wa Blackburn Andy McEvoy na John Byrom mnamo mwaka 1965.
Mpaka wakati timu zikiwa zimecheza mechi 28, McEvoy alikuwa kashafunga mabao 25 wakati John Byrom alikuwa kashafunga mabao 18.
Suarez mpaka sasa kashafunga mabao 24 na Sturridge 18.
0 comments:
Post a Comment