Searching...
Tuesday, March 25, 2014

Nafuu kwa Oxlade-Chamberlain na Gibbs

Refa Andre Marriner alikosea kwa kutoa kadi nyekundu: FA
Wachezaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Kieran Gibbs wameondolewa adhabu ya kadi nyekundu baada ya Gibbs kuondolewa uwanjani kimakosa wakati wa mchuano wa siku ya Jumamosi ambapo Arsenal ilishindwa vibaya na Chelsea kwa kipigo cha magoli 6-0 uwanjani Stamford Bridge.
Jopo la chama cha soka England, FA, limesema kuwa refa Andre Marriner alikosea kwa kumtimua uwanjani Kieran Gibbs na kwamba tukio la Oxlade-Chamberlain kuunawa mpira katika eneo la hatari haikustahili kadi nyekundu.
Sasa wachezaji hao hawatahudumia marufuku ya mechi kutokana na tukio hilo.
Maafisa wa usimamizi wa mechi walisema kuwa refa huyo mwenye umri wa miaka 43, ambaye tayari ameomba msamaha kwa kukanganya majina ya wachezaji, anapaswa kupewa fursa nyingine kurekebisha makosa yake badala ya kunyimwa kibarua mwishoni mwa juma hili

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!