Searching...
Wednesday, March 12, 2014

MAN UNITED YAFUNGUA MAZUNGUMZO NA SPORTING LISBON KUMSAJILI WILLIAM CARVALHO

Manchester United imefungua majadiliano na klabu ya Sporting Lisbon juu ya uhamisho wa kiungo mkabaji wa William Carvalho.
Meneja wa United David Moyes anaaminika kumuweka kiungo huyo mwenye miaka 21 katika listi ya wachezaji atakaowasajili kipindi dirisha la usajili litakpofunguliwa, hii ni kwa mujibu wa taarifa za usajili barani ulaya. 


Klabu ya Ureno imepanga kiasi cha €35million (£29m) kwa timu yoyote itakayomtaka kiungo huyo ambaye ana asili ya Angola, lakini United wapo tayari kulipa kiasi cha €35million.

Lakini kwa kuwa United wanataka kumaliza biashara yao ya usajili mapema kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia, wanaweza wakakubali kulipa fedha wanayotaka. 

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!