Mahakama
nchini Spain imeishtaki rasmi klabu bingwa ya nchi hiyo FC Barcelona
kwa kufanya udanganyifu wa fedha zaidi ya $12.5 million zilizotumika
katika uhamisho wa mshambuliaji wa kibrazil Neymar.
Judge
Pablo Ruz alisema maamuzi yake yamekuja kutokana kuwepo kwa ushahidi wa
kutosha juu ya mashtaka hayo yanayohusiana na uhamisho wa Neymar
uliogharimu kiasi cha 57 million euro kutoka Santos msimu uliopita.
Ruz pia ametoa amri ya kuchunguzwa kwa Raisi aliyejiuzulu wa klabu ya FC Barcelona Sandro Rosell juu ya uhamisho huo.
Rosell
alijiuzulu haraka baada ya kugundulika kiasi cha 40 million euros ($55
million) za uhamisho zililipwa kwa kampuni ya baba yake Neymar, ambaye
ameitwa kuja kutoa ushahidi mahakamani hapo.
Barcelona imeyakataa mashataka hayo.
0 comments:
Post a Comment