Golikipa
wa Bayern Munich Manuel Neuer amewaambia FIFA waachane na adhabu ya
mara tatu - penati, kadi nyekundu, na kusimamishwa mechi moja kwa
mchezaji ambaye atamzuia mwenzie nafasi ya kwenda kufunga kwa kucheza
rafu ndani ya penalty box.
Wakati
wa mchezo wa raundi ya 16 bora kati ya Arsenal na Bayern pale Emirates
Stadium, Wojciech Szczesny alimchezea rafu Arjen Robben, na akatolewa
nje kwa kadi nyekundu.
Ingawa
David Alaba alikosa penati, Bayern walifanikiwa kushinda 2-0 Szczesny
sasa ataukosa mchezo ujao pale Allianz Arena utakaochezwa March 11.
Hata hivyo Neuer anaamini kwamba kusababisha penati ni adhabu tosha - kutoa kadi nyekundu zaidi inakuwa ni adhabu kubwa.
“Inabidi
hili suala waliangalie vizuri, timu inakuwa ishapewa penati, kuongezea
kadi nyekundu inazidisha makali makubwa kwa adhabu hiyo. FIFA
waliangalie tena hili suala.
0 comments:
Post a Comment