Washabiki
wa mpira wa miguu nchini watashuhudia bure mechi ya timu ya Taifa ya
mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) dhidi ya Zambia (Shepolopolo).
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa
Wanawake (AWC) itachezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili
alasiri.
Twiga
Stars ambayo ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Lusaka, Februari 14
mwaka huu kwa mabao 2-1 iko kambini chini ya Kocha Rogasian Kaijage na
msaidizi wake Nasra Juma ikijiwinda kuwakabili Wazambia wanaotarajiwa
kutua nchini Alhamisi (Februari 26 mwaka huu).
Waamuzi
wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana
na Suavis Iratunga kutoka Burundi kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili
nchini keshokutwa (Februari 26 mwaka huu). Kamishna Fran Hilton Smith
kutoka Afrika Kusini yeye atatua nchini Februari 27 mwaka huu kwa ndege
ya South Africa Airways.
0 comments:
Post a Comment