Searching...
Sunday, May 5, 2013

RAIS KIKWETE WA TANZANIA AMPOKEA RAIS WA SERIKALI YA MPITO YA MADAGASCAR JIONI HII


Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili mjini Dar Es Salaam jioni ya leo , Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya
kikazi ya siku mbili.


Amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar
Es Salaam na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi hao wanatarajiwa kufanya  mazungumzo baadaye leo Ikulu,
Dar Es salaam.

Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi yaa Siasa, Ulinzi na
Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anakutana na Rais Rajoelina kwa mara ya tatu sasa, mara ya kwanza ikiwa ni mwezi Desemba mwaka jana, na baadaye mwezi Januari  mwaka huu.

 Rais Kikwete alipokutana mara ya mwisho na Rais huyo wa serikali ya mpito ya Madagascar alifanikiwa kumshawishi akubaliane na mapendekezo ya nchi za SADC kuwa asigombee kwenye uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka huu kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Rais Kikwete awali ya hapo aliweza pia kumshawishi  Rais wa zamani
wa Madagascar Mhe Marc Ravalomanana  asigombee katika uchaguzi  mkuu huo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013
Rais Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mhe. Andry Rajoelina aliyewasili jioni ya leo Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini,katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!