Searching...
Thursday, April 18, 2013

HUKUMU YA SHEIKH PONDA YAKUMBWA NA MIZENGWE MAHAKAMANI


HUKUMU ya Kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya maandamano haramu imeahirishwa mpaka tarehe 9 mei mwaka huu...
Kesi hiyo imeharishwa baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa ,kutokuwepo Mahakamani hapo...
Awali hakimu huyo alitarajiwa kuketi katika kiti cha enzi na kutoa hukumu ya kesi hiyo Na.245/2012 inayomkabili Ponda na wenzake. 
Aprili 3 mwaka huu:Mawakili wa upande wa Jamhuri ,Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi Juma Nassor  na Njama waliwasilisha majumuisho yao mahakamani hapo kwa njia ya maandishi ambapo mawakili wa upande wa jamhuri waliiomba mahakama iwaone washitakiwa wote wana hatia na wapewe adhabu kwa mujibu wa sheria.
Wakati mawakili wa utetezi waliiomba mahakama iwaone washitakiwa hawana hatia na iwaachilie huru kwa sababu hawakutenda makosa yanayowakabili na kwamba upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yao.
Edited:by Abuu

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!