Searching...
Wednesday, November 21, 2012

ROBERTO DI MATTEO ATIMULIWA KAZI CHELSEA

Roberto Di Matteo.
KOCHA wa muda wa Klabu ya Chelsea ya England, Roberto Di Matteo, leo ametimuliwa kazi kutokana na kichapo cha bao 3-0 kutoka kwa Juventus katika mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya jana.
Di Matteo aliyekuwa na mkataba wa miaka 2 na klabu hiyo, alichukua mikoba ya kocha, Andre Villas-Boas Machi mwaka huu.
Matteo alifanikiwa kutwaa kombe la Klabu Bingwa Ulaya pamoja na kombe la FA msimu uliopita akiwa na timu hiyo.
Klabu ya Chelsea itatangaza mtu atakayechukua mikoba ya kocha huyo aliyetimuliwa, japo kuna tetesi kuwa kocha wa zamani wa Liverpool, Rafael Benítez anaweza kuchukua nafasi hiyo baada ya kuwa katika mazungumzo na mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!