Searching...
Friday, November 2, 2012

NHIF YATOA SOMO KWA WANAVYUO NACHINGWEA

Mwakilishi wa NHIF na CHF Lindi Fortunata Kullaya akitoa elimu na uhamasishaji kwa wanachuo wa chuo cha ualimu Nachingwea kufahamu umuhimu wa kujiunga na Mfuko.
mratibu wa NHIF/CHF Abinery Mkanya kwa chuo cha ualimu Nachingwea akiwasilisha majina ya wanachama waliojiunga papo kwa papo kwenye meza ya uratibu wakati wa zoezi la uhamasishaji.
Mratibu wa CHF Wilaya ya Nachingwea Masiah Nyoni akifafanua maswali yaliyoulizwa kutoka kwa washiriki wa mafunzo ya elimu ya NHIF na Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) ambao ni wanachuo wa chuo cha ualimu Nachingwea (NTTC).
Fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni yanayohusu changamoto na maboresho katika NHIF na CHF yalitolewa,pichani ni Ally Ngilima mwanachuo wa mwaka wa kwanza chuo cha ualimu Nachingwea akitoa maoni.
Veronika Luanda akipewa maelekezo na mwakilishi wa NHIF Lindi Fortunata Kullaya wakati wa utekelezaji wa mpango wa elimu kwa wanachama wa NHIF,uliofanyika kwenye chuo cha Uuguzi Nachingwea (NTC).

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!