Searching...
Monday, October 8, 2012

Rick Ross apagawisha vilivyo Serengeti Fiesta 2012



Msanii maarufu wa Rick Ross kutoka nchini Marekani akishambulia jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo kubwa la burudani nchini pia lilitumbuizwa na wasanii kibao wa nyumbani.
 


 
 Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross akiimba jukwaani  usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.

 Mkali mwingine wa miduara AT na madansa wake wakilishambulia jukwaa.

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,akiimba jukwaani na shabiki wake.
 Mashabiki wakitaka kuangusha uzio uliowekwa kwa ajili ya usalama.
 Baadhi ya Askari wakijaribu kuweka usalama wa kutosha kwa Mwanamuziki Rick Ross imara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lidaz Club,kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 201.
 Viwanja vya Lidaz palikuwa hapatoshi hata kidogo.
 Mwanamuziki kutoka nchini Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini.
Watu kibao wakiwa ndani ya viwanja vya lidaz club usiku huu.
Msanii wa miondoko ya rusha rohoo a.k.a Miduara,Shilole akijiachia jukwaani vilivyo na madansa wake usiku huu mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye viwanja vya Lidaz Club,katika kuhitimisha kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!