Searching...
Friday, September 28, 2012

Majeshi ya AMISOM yaingia Kismayo


Majeshi Kismayo
Hatimaye wanajeshi wa Kenya wameuteka mji wa Kismayo.
Wanajeshi wa Kenya walifanikiwa kuingia mji huo baada ya kukabiliana vikali na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.
Msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Cyrus Oguna aliambia BBC kuwa wanajeshi wa Kenya kwa ushirikiano na wale wa Somalia walianza harakati zao mapema asubuhi ya leo.
Aliongeza kuwa hadi kufikia sasa Al Shabaab hawajakabiliana na jeshi hilo kuzuia kutekwa kwa mji huo.
Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa Al Shabaab husalimu amri kwa muda wakati wanapokabiliwa na majeshi yenye nguvu kuwaliko.
Ndege za kivita za Kenya zilifanya mashambulizi ya angani mapema wiki hii na kuharibu boharli lenye silaha za wapiganaji hao mjini humo.
Wiki iliyopita, Al Shabaab walijiandaa kuondoka Kismayo na hata kuwahamisha wapiganaji wao pamoja na silaha.
Mji huo wa bandarini ni muhimu kwa Al Shabaab kwani wanautumia kuingizia silaha na pia kuwatoza kodi wenyeji wa mji huo.
Hatua ya wao kupoteza mji huo, itakuwa ni pigo kubwa kwao, lakini wapiganaji hao wa Al Shabaab bado wana uwezo wa kufanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Somalia na wale wa Muungano wa Afrika hata katika sahamu ambazo wanajeshi hao wanadhibiti.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!