Steven Kiprotich wa Uganda amekishangaza kikosi kikali cha Wakenya na kushinda mbio za marathon kunako siku ya kuhitimisha michezo ya Olimpiki ya London 2012.
Kiprotich ameshinda mbio hizi katika mda wa saa 2 dakika 08 na sekunde 01 kupitia mitaa ya jiji la London akiwa mbele ya mshindi wa mara mbili wa mbio za marathon na bingwa mtetezi Abel Kirui aliyemaliza wa pili katika mda wa saa 2 dakika 08 na sekunde 27.
Mkenya mwingine aliyeongoza mbio za leo kwa kipindi kirefu Wilson Kipsang, ameshinda medali ya shaba akimaliza katika mda wa saa 2:09.37.
Mbio hizi kwa kipindi cha kilomita 10 kilitawaliwa na Franck De Almeida kutoka Brazil ikiashiria mbio kali zitakazowaniwa kati ya Wakenya na Waethiopia. Lakini mbinu za Ethiopia zilichachuka pale Dino Sefir alipoonekana kuishiwa nguvu na kasi yake kupungua na Kipsang kuanza kuwasha moto na kuongoza kupitia mitaa kadhaa ya Jiji.
Mkenya huyu aliweka pengo la sekunde 30 kupitia eneo ambalo lina vivutio safi vya mji wa London na kufikia kituo cha kilomita 30 mwanariadha wa pili wa Ethiopia Getu Feleke akaonyesha dalili za kukata tamaa na kuonekana kurudi nyuma.
Kufikia eneo lilikua na watazamaji wengi sana Kiprotich akaongezea mafuta miguu na kuanza kumkimbiza Kipsang akigawanya kikundi cha wakimbiaji waliokua wakisaka nafasi nono za medali.
Hatua yake ilisababisha kuwaamsha Wakenya, kwanza mshindi wa Marathon za Dubai Ayele Abshero wa Ethiopia aliyepunguza pengo lililowekwa na Kipsang hadi sekunde 11 na kufikia kilomita 25 walikua pamoja.
Kundi lililokua likiongoza kupitia sehemu iliyofunikwa ya soko la Leadenhall kuingia hatua ya kilomita saba za mwisho, Wakenya walijitahidi kumuacha Kiprotich.
Lakini Kiprotich akiwaonelea wa Kenya walio mbele yake wakisinzia na kuweka kasi yake juu na kuwapita kwenye hatua ya kilomita 32 na kuwashangaza alipowaacha kwa tofauti ya mita 200.
Kiprotich, ambaye alihamisha mazowezi yake katika eneo maarufu la mazowezi huko Eldoret ambako amejiunga na bingwa wa zamani wa mbio za mita 5000 Eliud Kipchoge, aliongezea kasi yake na kudhibiti nafasi yake mbele.
Kupitia kilomita mbili za mwisho, Mganda huyo mwenye umri wa miaka 23 alikua mbele ya Kirui kwa tofauti ya sekunde 20 na aliweza kupata mda wa kuchungulia anayemfuta yuko wapi kabla ya kunyakua bendera ya Uganda kwenye hatua yake ya mwisho akiingia Mall, pembezuni mwa Kasri ya Buckingham, na kuivaa shingoni wakati akivuka mstari wa kumalizia mbio hizi.
Kumaliza mbio
1 Kiprotich UGA 2:08:01 - Dhahabu
2 Kirui KEN 2:08:27 - Fedha
3 Kiprotich KEN 2:09:37 - Shaba
0 comments:
Post a Comment