
Malkia Elizabeth mwenye umri wa miaka 86 na familia yake waliwapungia mikono wakazi wa London huku wakipeperusha bendera za nchi hiyo kutoka kwenye eneo la nje Jumanne wakati ndege ya kifalme ikiruka angani.
Wakati huo huo Rais Barack Obama wa Marekani alitoa salamu binafsi kwa malkia akisema anamatumaini ataendelea kuongoza na kuwa na afya salama kwa miaka mingi ijayo. Katika video iliyotolewa kwenye tovuti ya White House bwana Obama alimuita malkia “living witness” kwa kuboresha uhusiano maalumu kati ya Uingereza na Marekani, dhamana ambayo alisema inabaki kuwa muhimu sana kwa nchi zao hizo mbili na dunia.
0 comments:
Post a Comment