Searching...
Sunday, January 1, 2012

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli Atangaza Ongezeko La Viwango Vya Nauli Katika Vivuko Vyote Vya Serikali Nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Herbert Mrango (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (katikati) alipokutana na waandishi wa habari hawapo pichani jijini leo na kutoa taarifa kuhusu ongezeko la viwango mbalimbali vya nauli katika vivuko nchini , (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA Prof, Idrissa Mshoro.
Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli (kushoto) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani Jan, I, 2011 jijini Dar es Salaam kuhusu ongezeko la viwango vya nauli katika vivuko. Wizara ya Ujenzi kuanzia tarehe 1 Januari kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imeongeza viwango vya nauli katika vivuko vyote vya serikali nchini, (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA Profesa Idrissa Mshoro,
Waziri wa Ujenzi Dakt. John Pombe Magufuli (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Jan, 1,2012 kuhusu ongezeko la viwango vya nauli katika vivuko vyote vya serikali nchini, ambapo kuanzia Jan, 1 ,2012, Wizara yake kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imeongeza viwango vya nauli kutokana na maeneo mbalimbali ya vivuko, , amezitaja nauli hizo kwa mfano MV. Magogoni na Mv. Kigamboni kwa Mkoa wa DSM ni kati ya shilingi 200 kwa watu wazima , watoto chini ya miaka 14, shilingi 50, na wanafunzi waliovaa sare za shule na vitambul;isho ni bure, Pia akatoa mfano wa Kivuko cha MV. Chato kitatoza nauli ya watu wazima shilingi 3,000/, watoto chini ya miaka 14 ni elf 50 ,na wanafunzi wenye sare za shule ni bure. Bei hizi zimepanda kutokana na gharama kupanda za uendesaji. (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA Prof, Idrissa Mshoro. (kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Herbert Mrango.Picha na Mwanakombo Juma-Maelezo

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!