Searching...
Thursday, December 22, 2011

MAAFA YA MAFURIKO DAR ES SALAAM HALI NI YA KUSIKITISHA


Hali ni mbaya katika barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ambapo kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiishi hapo, japokuwa serikali imekuwa ikiwaambia hawatakiwa mkujenga katika eneo hilo kutokana na madhara yanayoweza kutokea endapo mvua zitanyesha,Lakini hali ndivyo ilivyo kwa sasa, ambapo katika eneo hilo maji yamefurika nyumba zinaelea kwenye maji na barabara hiyo imefunikwa na maji na kusababisha vyombo vya usalama kuifunga, hivyo kukata mawasiliano kati ya Kariakoo na mjini maeneo na Magomeni. Kutokana na nvua ambayo imenyesha siku mbili mfurulizo jijini Dar es salaam Watu ni wengi katika eneo hilo lakini pia kutokana na ubishi, kunawatu wamekuwa wakizolewa na maji kwa sababu ya kulazimisha kuvuka, wakati maji hayo yanaenda kwa kasi kubwa, baadhi ya watu wamekuwa wakiokolewa na vikosi vya uokoaji na wanapelekwa katika hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi, kama wanavyoonekana wakina mama hawa katika picha wakipelekwa kwenye gari baada ya kuokolewa kwenye maji.

 
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa kushoto amekuwepo pia katika tukio hilo la uokoaji, hapa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanausalama

 
Hapa ni mahali ambapo pamewekwa uzio ili kuzuia watu kuvuka ng'ambo yaani uapnde wa pili.
 
Baadhi ya watu wakiokooa vitu vyao na kuviweka kando ya barabara ya Morogoro.
 
Hawa wajapan wanaofanya kazi katika kampuni ya Kajima yenye ofisi zake hapo Jangwani ambayo nayo imevamiwa na maji na kuharibu vitu mbalimbali huku maji yakiwazingira baadhi ya wafanyakazi ambao walikuwa wakiokolewa na vikosi wa uokozi.
 
Baadhi ya nyumba zikiwa zimezingirwa kabisa na maji katika eneo la Jangwani.
 
Baadhi ya watu wamekuwa wakikimbilia kwenye mapaa ya nyumba kama nyumba zinavyoonekana zikiwa zimezama kabisa kwenye maji.
 
Eneo lote la Jangwani limebadilika na kuwa kama ziwa vile kutokana na mafuriko
 hayo
Chanzo: http://fullshangwe.blogspot.com/

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!