Searching...
Sunday, August 21, 2011

Ubalozi Wa Tanzania Nchini Uingereza Waandaa Futari

Carol kutoka ubalozini(kushoto) akila pozi na jestina George.
Afisa Zamarani akiwakaribisha wadau wote.
ustaadhi akiangalia mda kama umefika ili wadau wapate kufuturu.
Aziza Ongala( Mtoto wa hayati Remmy Ongala) Akila pozi na Frank.
Mh Naibu Balozi kilumanga akitoa shukrani kwa wote walioweza kuja kupata futari .
Mzee Kiondo kutoka Ubalozini akisubiria Futari.
Freddy Macha katikati akiwa na wadau.
hata watoto walikuwepo.
Futari likikwenda sambamba kwa kupiga stori na kufurahia
wadau wakipata Futari.
muda wa kupata futari ndio huu.
wakati wa dua.
-----
Salaam,

Ubalozi wa Tanzania Hapa London Leo uliwaalika watanzania wote kutoka madhehebu na dini mbalimbali kuja kupata futari ya pamoja walioandaa ikiwa ni ishara njema ya kuonyesha amani,upendo, ukarimu kwa watanzania wote. Vyakula vya aina mbalimbali viliandaliwa  na vilipikwa katika hadhi ya kitanzania. Naibu Balozi Mh Chabaka aliwashuru wadau wote ambao waliweza kuja na kujumuika na kufuturu kwa pamoja. Aidha Mh Balozi aliahidi kushirikiana na watanzania kwa ukaribu zaidi katika hali na mali pia kuwaomba kutoa ushirikiano wao na ubalozi katika kuboresha mawasiliano na utendaji wa kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Aliendelea kwa kusema Ubalozi upo kwa ajili yetu hivyo tuutumie ipasavyo.


Kwa niaba ya URBAN PULSE CREATIVE Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ubalozi wetu kwa namna walivyojitolea kutengeneza futari na kuwakaribisha wadau kuja kufuturu.

Asanteni Sana,

MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

URBAN PULSE CREATIVE

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!