Searching...
Sunday, August 21, 2011

AIRTEL YAMWAGA MSAADA WA VITABU SUA SEKONDARI


Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Tunu Kavishe (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari SUA, Rogers Shempemba vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Pwani, Aluta Kweka na Mkuu wa Sekondari ya SUA, Khalfan Millongo. Pichani juu: Meneja Mauzo  Kanda ya Pwani wa kampuni ya simu ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Sekondari ya SUA, Khalfan Millongo, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tunu Kavishe na Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya. Vitabu hivyo vina thamani ya shs milioni 4.
 
Meneja Mauzo  Kanda ya Pwani wa kampuni ya simu ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari SUA, Happiness Makundi vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe na kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo. Vitabu hivyo vina thamani ya shs milioni 4.
 
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Tunu Kavishe (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari SUA, Rogers Shempemba vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Pwani, Aluta Kweka na Mkuu wa Sekondari ya SUA, Khalfan Millongo na kulia kabisa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo.
 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo (kulia) akimshukuru Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) katika hafla ambayo Airtel ilikabidhi msaada wa vitabu vyenye thamani ya shs milioni 4  kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkuu wa Shule ya Sekondari SUA, Khalfan Millongo.
 
Meneja wa Kanda ya Pwani wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto) akipeana mikono na Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo katika hafla ambayo Airtel ilikabidhi msaada wa vitabu vyenye thamani ya shs milioni 4  kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe na Mkuu wa Shule ya Sekondari SUA, Khalfan Millongo.
 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Alfred Shayo, akihutubia katika hafla ambayo Airtel ilikabidhi msaada wa vitabu vyenye thamani ya shs milioni 4  kwa Shule za Sekondari za SUA, Mwembesengo, Mji Mpya na Mgulasi Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe na Mkuu wa Shule ya Sekondari SUA, Khalfan Millongo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!