Searching...
Tuesday, July 5, 2011

Gabon kuanzisha mafunzo ya Kiswahili mashuleni

 Tanzania imeombwa kuisaidia Gabon kubuni, kuanzisha na kusimamia mitaala inayofaa kuanzisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika shule za nchi hiyo kutokana na uamuzi wa Serikali ya Gabon kuanza kufundisha lugha hiyo tangu elimu ya msingi. Aidha, Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba amemwomba binafsi Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kusaidia kumpatia mwalimu binafsi wa kumfundisha lugha ya Kiswahili ikiwa ni jitihada zake za kuonesha mfano wa kuimarisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili kwa wananchi wake.
Gabon inakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kukumbatia na kuamua kufundisha Kiswahili shuleni nje ya nchi za Jumuiya ya Mashariki za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda hata kama lugha ya Kiswahili inazungumzwa na mamilioni ya watu nje ya eneo la Jumuiya hiyo ndani na nje ya Afrika.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!