Searching...
Thursday, May 12, 2011

Ban Ki-moo ataka kusimamishwa mapigano nchini Libya

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kusimamishwa mapigano mara moja nchini libya. Ban Ki-moon amesema serikali ya Kanali Muammar Gaddafi wa Libya imekubali kuruhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa kutembelea Libya. Amesema kuwa amezungumza na Waziri Mkuu wa Libya Baghdadi Al-Mahmoudi ili kuhimiza suala la kusimamishwa mapigano na kutaka wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa waruhusiwe kwenda nchini humo bila ya kizuizi chochote. Ban Ki-moon pia ameitaka serikali ya Gaddafi kuacha kuwashambulia raia. Ameongeza kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Abdul Ilah Khatib ataelekea Libya kujadili suala la kukomeshwa mgogoro wa nchi hiyo kwa njia za amani.
Wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kusimamishwa mapigano nchini Libya umetolewa huku ripoti zikisema kuwa wanamapinduzi wanaopinga serikali ya Muammar Gaddafi wamefanikiwa kutwaa uwanja wa ndege wa mji wa Misratah magharibi mwa nchi hiyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!