Searching...
Thursday, April 21, 2011

Viongozi wa Afrika Mashariki wataka misaada zaidi itumwe nchini Somalia

 Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa misaada zaidi ya kifedha kwa ajili ya kikosi cha Umoja wa Afrika cha Kulinda Amani Somalia AMISOM.
Katika taarifa ya pamoja waliyotoa leo mjini Dar-es-Salaam Tanzania baada ya kumalizika mkutano wao wa 9 wa kilele, viongozi hao wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia kujiimarisha katika kurejesha amani na kukabiliana na waasi wa al-Shabab.
Viongozi hao wamezipongeza nchi za Afrika ambazo zimetuma vikosi vya kulinda amani nchini Somalia.
Katika taarifa yao, viongozi hao wamemteua katibu mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr. Richard Ssezibera wa Rwanda kwa kipindi cha miaka mitano. Katibu Mkuu wa sasa Juma Mwapachu kutoka Tanzania atastaafu baadaye mwezi huu baada ya kuhudumu kwa muda wa miaka mitano. Kikao hicho cha Dar-es-Salaam kimedhudhuriwa na mwenyeji Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, mwenyekiti wa sasa wa jumuiya hiyo Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa Rwanda Bernard Makuza.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!