Searching...
Wednesday, April 6, 2011

Kikosi kitiifu kwa Laurent Gbagbo wa Ivory Coast chasalimu amri

 Askari wa kiongozi anayeendelea kung'ang'ania uongozi nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo wametangaza kusitisha vita nchini humo na kutoa ombi la vita hivyo kusimamishwa. Mkuu wa kikosi cha Gbagbo, Jenerali Philippe Mangou amesema kuwa, askari wake wamesitisha mashambulizi yao na kuvitaka vikosi vya Umoja wa Mataifa na Ufaransa vinavyokiunga mkono kikosi cha Alassane Outtara, kiongozi anayetambulika na jamii ya kimataifa kuwa rais halali wa Kodivaa visimamishe mashambulizi yao. Hapo jana, helikopta za UN na za Ufaransa zilifanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Gbagbo na hata kuishambulia ikulu ya kiongozi huyo mjini Abidjan. Hata hivyo, Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa UN amesema kuwa vikosi vya umoja huo vimelazimika kufanya mashambulizi hayo ili kuwalinda raia na jinai zinazofanywa na vikosi vitiifu kwa Gbagbo na kuongeza kwamba, mashambulizi hayo hayana maana kwamba UN imejiunga na vita vya kumng'oa Gbagbo madarakani.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!