Searching...
Sunday, May 1, 2011

Gaddafi anataka mazungumzo

Kiongozi wa Libya, Kanali Gaddafi, ametoa wito kwa Nato kwamba kufanywe mazungumzo ili kusimamisha mashambulio ya ndege za umoja huo dhidi ya nchi yake.
Katika hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni, Kanali Gaddafi alisema yeye yuko tayari kusimamisha mapigano ikiwa itakubaliwa na pande zote.
Mlibya anatazama hotuba ya Kanali Gaddafi
Katika hotuba yake Jumamosi asubuhi, kiongozi wa Libya alisema yuko tayari kutoa amri kuwa mapigano yasitishwe na kuanza mazungumzo, endapo NATO itaacha mashambulio ya mabomu.
Lakini alikataa lile dai kubwa la wapiganaji na jumuiya ya kimataifa, kwamba yeye aondoke.
Alisema hatong'atuka wala kuihama Libya.
Wengi serikalini wanaona kuwa wameshakaribisha mazungumzo kwa kukubali mpago wa Umoja wa Afrika wa kurejesha amani; lakini wanahisi upinzani ndio hautaki kumaliza mapigano, kwa sababu unakataa kuzungumza na serikali ya Kanali Gaddafi.
Alipokuwa Kanali Gaddafi anazungumza, NATO ilidondosha makombora matatu mjini Tripoli, kwenye yale yaliyoonekana kama majengo ya serikali.
Hotuba ya Kanali Gaddafi, ilikuwa mchanganyiko wa kukaza na kulegeza kamba.
Alisema kila mwananchi wa Libya sasa anakabili mambo mawili : uhuru ama kifo.
Hakuna kusalliam amri, hakuna hofu wala kuondoka.

1 comments:

Dr. Iglesias said...

Vita ya Libya. NATO unaua Gaddafi mwana mdogo na wajukuu watatu. Urusi ni kujiandaa kwa vita ya nyuklia ... Kuangalia kwa:

http://aims.selfip.org/~alKvc74FbC8z2llzuHa9/default_libia.htm

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!