Searching...
Friday, March 25, 2011

Tetemeko la ardhi lililotokea nchini Myanmar lasababisha vifo vya watu 65



Habari kutoka serikali ya Myanmar zimesema, tetemeko kubwa la ardhi lililotokea usiku wa tarehe 24 kaskazini mashariki mwa Myanmar, limesababisha vifo vya watu 65.
Idara ya hali ya hewa ya Myanmar imesema tetemeko hilo lilikuwa lenye nguvu ya 7 kwa kipimo cha richer. Tetemeko hilo lilisababisha uharibifu mkubwa wa nyumba na barabara mjini Tachilek, na watu wengi kujeruiwa. Maofisa wa serikali wanasema kwa kuwa sio watu wengi wanaoishi katika sehemu ya kiini cha tetemeko hilo, hivyo uwezekano wa kutokea vifo na majeruhi mengi zaidi ni mdogo.
Rais Hu Jintao wa China ametuma salamu za rambirambi kwa rais U Thein Sein wa Myanmar.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!