Searching...
Friday, March 25, 2011

Polisi ya Kenya yaiomba bunge kubuni Mahakama ya kupambana na mihadarati

 Kamishna wa Polisi ya Kenya Mathew Iteere ametoa wito kwa kamati ya bunge inayoshughulikia usalama wa taifa kuwasilisha muswada wa kubuniwa kwa mahakama maalumu ya kusikiliza kesi zinazohusiana na ulanguzi wa dawa za kulevya. Iteere amewaambia wabunge kuwa kesi zinazohusiana na mihadarati hukabiliwa na changamoto kutokana na ukosefu wa sheria kali za kupambana na kadhia hiyo. Kamishna wa polisi pia amewataka wabunge kupitisha sheria itakayopandisha kiwango cha fedha zinazotolewa kama dhamana kwa washukiwa wa mihadarati kwani ada ya dhamana hiyo kwa sasa ni ya chini na kwa mantiki hiyo walanguzi huweza kujilipia mara moja na kuondoka korokoroni. Mathew iteere amesema jeshi la polisi ya Kenya limejitahidi kuimarisha doria katika mipaka ya nchi hiyo ili kukabiliana na ulanguzi wa mihadarati.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!