Searching...
Friday, March 25, 2011

Mionzi ya nyuklia yatishia usalama wa chakula nchini Japan


Eneo lililoathiriwa na mionzi ya nyukilia kutoka kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia cha Fukushima nchini Japan limezidi kupanuka. Waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Naoto Kan kwa mara ya kwanza amewataka wananchi wa Japan wasile aina kadhaa za mboga kutoka sehemu ya Fukushima.
Wizara ya utamaduni na sayansi ya Japan imetangaza kuwa mionzi ya nyukilia kwa maji ya bomba umegunduliwa katika sehemu 11 nchini Japan.
Nchi nyingine zinazoagiza mazao ya kilimo kutoka kwenye Japan zimeongeza ukaguzi, na hata baadhi ya nchi hizo zimesimamisha ununuzi wa mazao ya kilimo kutoka Japan.
Habari nyingine zinasema shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA limesema hali ya hamasa imeonekana baada ya kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Fukushima kuunganishwa tena na mtandao wa umeme, lakini kwa ujumla hali ya huko bado inakabiliwa na changamoto kubwa.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!