Searching...
Saturday, March 5, 2011

Libya yateua mwakilishi mpya UN, mapigano yapamba moto

Libya imemteua Ali Abdulassalam Treki waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kuwa mwakilishi mpya wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa.
Treki atachukua nafasi ya mwakilishi wa zamani wa Libya katika umoja huo ambaye ametangaza kumpinga Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba, Libya ina haki ya kuchagua mwakilishi wake katika umoja huo.
Hata hivyo haijulikani kama Marekani itakubali kumpa visa balozi huyo mpya wa Libya katika Umoja wa Mataifa au la.
Wakati hayo yakiripotiwa vikosi vya Gaddafi vimeshambulia ghala la silaha katika mji wa Benghazi na kupelekea watu 16 kuuawa.
Hayo yanajiri huku askari waliokataa kumtii Gaddafi wakiendelea kupambana vikali na vikosi vinavyomuunga mkono kiongozi huyo wa Libya.
Wapinzani wa Libya wameipotiwa kudhibiti mji muhimu wenye mafuta wa nchi hiyo wa Raslanuf jana Ijumaa.
Wakati huo huo imeripotiwa kuwa Muammar Gaddafi ameajiri mamia ya mamluki kutoka nchini Mali kupambana na wananchi wake wanaompinga.
Inasemekana kuwa Gaddafi anawalipa mamluki hao wa jamii ya Tuareg kutoka Mali mshahara wa dola elfu 10 ili kushiriki kwenye mauaji hayo na anampa kila mmoja marupurupu ya dola 1,000 kila siku wanayopigana vita.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!