Searching...
Thursday, March 10, 2011

A. Kusini, India na Brazil zasisitiza udharura wa kufanyiwa marekebisha Umoja wa Mataifa

 Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Brazil na India wamesisitiza udharura wa kubadilishwa mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kuwe na tadbiri inayokubalika na nchi zote za dunia. Kwenye mkutano wa kamisheni ya pamoja ya nchi hizo tatu mjini New Delhi, viongozi hao wamesema kuwa mfumo ulioko kwa sasa ni wa kibepari na kwamba nchi chache zinahodhi uhuru wa dunia. Miongoni mwa mambo ambayo nchi hizo zinataka yatazamwe upya ni kura ya veto. Brazil imesema kuwa kura hiyo inapaswa kuondolewa na badala yake kuundwe mfumo utakaotoa nafasi sawa kwa nchi zote za dunia kushiriki katika kupitisha maamuzi muhimu ya Umoja wa Mataifa. Wito wa nchi hizo tatu unafanana na wito ambao umekuwa ukitolewa mara kwa mara na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na umedhihirisha wazi ari na utashi wa nchi za dunia kutaka mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!