Searching...
Wednesday, February 9, 2011

Serikali ya Misri na makundi ya upinzani wakubali kuunda kamati ya kutafiti mageuzi kuhusu katiba ya nchi

Makamu wa rais wa Misri Omar Suleiman amefanya mazungumzo na makundi ya upinzani, ambapo pande mbili zimekubaliana kuunda kamati ya kutafiti mageuzi yanayotakiwa kufanyika katika katiba ya nchi na utungaji wa sheria.
Taarifa iliyotolewa baada ya mazungumzo hayo inasema, kamati hiyo itaundwa na wanasheria na wanasiasa kabla ya mwezi Machi. Taarifa imesema, makundi ya upinzani yamekubali rais Mubarak kutogombea tena urais mwezi Septemba, na kuhakikisha mpito wa amani na uchaguzi mkuu utafanyika kwa uhuru na haki.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mchakato wa kukabidhiana madaraka nchini Misri unapaswa kuamuliwa na wananchi wa nchi hiyo na ufanyike kwa amani na utaratibu, ili kuepusha kuvuruga amani na utulivu katika Mashariki ya Kati.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!