Searching...
Thursday, February 24, 2011

Obama alaani ghasia nchini Libya

Eneo la Benghazi nchini Libya
Rais Barrack Obama wa Marekani amelaani machafuko yanayo endelea nchini Libya, katika hotuba yake ya kwanza kwenye runinga tangu mageuzi yaanze nchini Libya, yapata wiki moja sasa.

Amesema kuwa ukatili unaotumiwa na vyombo vya serikali kukabili waandamanaji haukubaliki kamwe na kuwa serikali yake inatathhmini hatua za kuchukua.
Japo hakutoa maelezo zaidi, alidokeza kuwa waziri wa mashauriano ya nje Hillary Clinton atasafiri mjini Geneva, Uswizi, kushauriana na nchi zingine.
Rais Obama akizungumza kuihusu Libya
Huku hayo yakiarifiwa maelfu ya waandamanaji wanaopinga serikali wamekuwa wakisherehekea kile wanachokiita ushindi mkubwa Mashariki mwa Libya.
Wakaazi mjini Tripoli wamesema wanaogopa kutoka nje kwa sababu wana wasiwasi wanajeshi wanaounga mkono serikali huenda wakawafyatulia risasi.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema yamethibitisha kuwa watu wasiopungua mia tatu wameuwawa tangu makabiliano hayo kuanza wiki iliyopita

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!