Robert Zoellick Mkuu wa Benki ya Dunia amesema kuwa ulimwengu unakabiliwa na ongezeko kubwa la bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu na kwamba nchi nyingi zinapaswa kuchukua hatua ili kukabiliana na ongezeko hilo la bei. Zoellick amewataka viongozi wa nchi za kundi la 20 kutoa kipaumbele cha kwanza kwa suala la chakula ili kupunguza bei ya bidhaa hiyo, ambayo inatishia hali ya wananchi maskini na kuzidisha gharama za maisha katika nchi zinazoendelea hususan za Asia na Afrika. Mkuu wa Benki ya Dunia amesema kuwa ulimwengu utakabiliwa na kupanda kwa bei za bidhaa zikiwemo za vyakula. Amesema kuongezeka kwa mahitaji ya vyakula kama vile sukari na nyama katika nchi zenye chumi zinazokuwa kwa kasi ni sababu kuu iliyopelekea kupanda kwa bei za vyakula hivi sasa katika nchi nyingi duniani ikilinganishwa na kupanda kwa bei hizo mwaka 2007 na 2008.Mkuu wa Benki ya Dunia ataka kupunguzwa bei za vyakula
Robert Zoellick Mkuu wa Benki ya Dunia amesema kuwa ulimwengu unakabiliwa na ongezeko kubwa la bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu na kwamba nchi nyingi zinapaswa kuchukua hatua ili kukabiliana na ongezeko hilo la bei. Zoellick amewataka viongozi wa nchi za kundi la 20 kutoa kipaumbele cha kwanza kwa suala la chakula ili kupunguza bei ya bidhaa hiyo, ambayo inatishia hali ya wananchi maskini na kuzidisha gharama za maisha katika nchi zinazoendelea hususan za Asia na Afrika. Mkuu wa Benki ya Dunia amesema kuwa ulimwengu utakabiliwa na kupanda kwa bei za bidhaa zikiwemo za vyakula. Amesema kuongezeka kwa mahitaji ya vyakula kama vile sukari na nyama katika nchi zenye chumi zinazokuwa kwa kasi ni sababu kuu iliyopelekea kupanda kwa bei za vyakula hivi sasa katika nchi nyingi duniani ikilinganishwa na kupanda kwa bei hizo mwaka 2007 na 2008.

0 comments:
Post a Comment