Searching...
Wednesday, February 16, 2011

Misri yazitaka nchi za Ulaya na Marekani kuzuia mali za Mubarak

 

Misri imeziomba nchi za Ulaya na Marekani kuzizuia akiba za benki za aliekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak. Nchi kadhaa ikiwemo Ujerumani zimethibitisha zimelizipokea ombi hilo na zimeahidi kufanya uchunguzi.

 

Kwa mujibu  wa  taarifa   ya  shirika la  habari la Ujerumani DPA, Misri imetoa ombi kwa nchi za Umoja wa Ulaya la kuzizuia    akiba za benki  za aliekuwa  rais nchi  hiyo Hosni Mubarak.Shirika hilo limezinukulu duru  za kidiplomasia za Umoja  wa  Ulaya.  Mawaziri wa Umoja  huo leo watakutana kulijadili ombi hilo la Misri.
Ombi hilo limetolewa kwa Uingereza,Ujerumani na Ufaransa la kuzizuia fedha   za viongozi wa ngazi  za  juu wa utawala wa  Mubarak.
Waziri wa mambo ya nje   wa Uingereza William   Hague amesema nchi yake italizangatia ombi hilo na  kwamba itachukua hatua madhubuti na za haraka endapo patapatikana  ushahidi juu ya wizi  wa  fedha za serikali ya Misri.
Akizungumza  bungeni  waziri Hague alisema kuwa serikali  ya Uingereza imepokea ombi kutoka   kwa serikali ya Misri la kuzikamata mali  za  viongozi  kadhaa  waliokuwamo katika utawala   wa  Rais  Hosni Mubarak.
Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle (Kulia), na William Hague wa Uingereza Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle (Kulia), na William Hague wa UingerezaWaziri  Hague  aliliarifu bunge  kuwa Uingereza  tayari imeshakua  hatua kama hiyo kuhusiana na Tunisia baada ya rais  wa nchi hiyo Zine El  Abidine Ben Ali kupinduliwa na  watu  wake.  Amehakikisha  kwamba Uingereza itashirikiana  na nchi  nyingine  za Umoja  wa  Ulaya  na washirika  wake wa kimataifa  katika  kulitekeleza ombi la Misri.
Mawaziri wa Umoja wa  Ulaya  leo watakutana mjini Brussels  kulijadili   ombi  la Misri,  Na  waziri  Mkuu  wa Luxemburg Jean-Claude  Juncker   amezitaka  nchi  za Umoja  wa Ulaya  ziige hatua  iliyochukuliwa na Uswisi ya kuzizuia  mali za Mubarak.
Ujerumani  pia imesema  kuwa  imelipokea ombi la Misri la  kuzitia kufuri akiba  za benki za viongozi wa serikali  na wabunge  wa Misri  waliokuwamo katika utawala  wa Mubarak.
Lakini Uingereza ndiyo  hasa  ipo  chini ya shinikizo  la kuchukua hatua  dhidi ya  mali za Mubarak na familia yake kutokana namadai  kwamba Mubarak na watu  wake wameficha  mamilioni  ya  fedha nchini Uingereza. 

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!