Searching...
Wednesday, February 16, 2011

Kenya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa nimonia

 Kenya leo imekuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuanza kutoa chanjo mpya dhidi ya ugonjwa wa nimonia kwa watoto ambayo inatarajiwa kuokoa maisha ya watoto nusu milioni walio chini ya umri wa miaka mitano nchini humo. Sherehe za kuanza kutolewa chanjo hiyo zimefanyika mjini Nairobi na kuhudhuriwa na Rais Mwai Kibaki huku mamia ya watoto wakipewa chanjo hiyo kwa mara ya kwanza.
Anthony Lake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF amesema kuwa, chanjo hiyo ya pneumococcal inaweza kusaidia kupunguza idadi ya watoto wanaofariki dunia kutokana na maradhi ya nimonia ambayo huua mamilioni ya watoto kila mwaka duniani na hasa katika nchi zinazoendelea.
Shirika linalosimamia chanjo na kinga ya mwili la GAVI Alliance limeazimia kuanza kutoa chanjo hiyo katika nchi 19 zinazoendelea duniani katika kipindi cha mwaka mmoja, miongoni mwa nchi hizo ni Nicaragua, Guyana, Yemen na Sierra Leone. Shirika hilo lina matumaini kuwa ifikapo mwaka 2015 nchi 40 duniani zitakuwa zikitoa chanjo hiyo kwa watoto.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!