Searching...
Monday, January 10, 2011

Ndege ya Iran Air yaanguka milimani

Idadi ya watu 77 wameuawa na wengine 35 wamejeruhiwa katika ajali ya ndege iliyotokea kutokana na  hali mbaya ya hali ya hewa, kaskazini-magharibi ya Iran.

Ndege hiyo ya Boeing 727 ya shirika la ndege la serikali Iran Air,ilianguka ilipokuwa ikijaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa mji wa Urumiyeh ulio katika eneo la milimani. Wakati wa ajali hiyo kulikuwepo dhoruba kali ya theluji na ukungu mzito. Ripoti zinasema kuwa rubani wa ndege hiyo, hapo awali aliripoti kuhusu tatizo la kiufundi.Ndege hiyo ilitokea mji mkuu wa Iran, Teheran.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!